Wakaazi wa jengo moja Kiambu watakiwa kuhama baada ya kuta za jengo kupasuka

  • | K24 Video
    2 views

    Zaidi ya wakaazi 20 wa jengo moja eneo la Kiamumbi kaunti ya Kiambu wametakiwa kuhama baada ya kuta za jengo hilo kupasuka na kuanza kuzama. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa jengo hilo, gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi ameahidi kuwa serikali ya kaunti itawasaidia wale watu walioathirika. Haya yanajiri huku waalimu wa shule za upili za awali wakiendelea kugoma na kushinikiza serikali kuwaajiri kwa kandarasi za kudumu kama walimu wengine.