Mawaziri Mutua na Tuya waongoza shughuli ya upanzi wa miti Mwingi

  • | Citizen TV
    246 views

    Mawaziri Alfred Mutua wa utalii na mwenzake Soipan Tuya wa mazingira wameongoza shughuli ya upanzi wa miti katika msitu wa Mumoni eneobunge la Mwingi kaskazini.

    Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mutua amesema kuwa lengo la upanzi wa miti ni kuafikia miti bilioni 15 kufikia mwaka wa 2032 kama alivyoahidi rais william ruto ili kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi. Mawaziri wamepewa jukumu la kuongoza upanzi wa miti kila mwezi katika kaunti mbalimbali. Miche milioni nne imepangiwa kupandwa katika kaunti za Taita Taveta na Kitui kufikia mwaka ujao.