Polisi wavamia Chuo Kikuu cha Columbia kutokana na maandamano

  • | BBC Swahili
    318 views
    Mamia ya waandamanaji wamekamatwa wakati wa operesheni ya usiku katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York City. Waandamanaji wanaounga mkono Palestina walikuwa wametawala jengo la chuo hicho hapo awali. Idara ya Polisi ya New York inasema jengo na hema lililokuwa chuoni hapo limesambaratishwa. Wakati huo huo, waandamanaji wanaounga mkono Israel walikabiliana na waandamanaji katika kambi zinazounga mkono Palestina huko Los Angeles, saa chache baada ya polisi kutawanya maandamano ya huko New York. Vyuo vikuu vya Marekani vimekuwa na maandamano huku wanafunzi wakidai kususia makampuni na watu binafsi wenye uhusiano na Israel wakati wa vita huko Gaza. #bbbcswahili #marekani #gaza Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw