Volcano ya Mlima Ibu Mkoa wa North Maluku yalipuka

  • | VOA Swahili
    175 views
    Volcano ya Mlima wa Ibu Indonesia katika kisiwa cha Halmahera kilicho mbali imeripuka Jumatatu (Mei 13) asubuhi, ikirusha majivu mazito rangi ya kijivu kilomita kadhaa angani, shirika linalotafiti milipuko ya volcano limesema. Volcano hiyo ililipuka majira ya saa tatu na dakika kumi na mbili asubuhi (0012GMT) kwa dakika tano, ikitupa majivu angani yenye rangi ya kijivu umbali wa kilomita 5 (maili 3.1), maafisa walieleza. Mlipuko mdogo ulirekodiwa katika eneo hilo Ijumaa (Mei 10). - Reuters #volcano #mlipuko #mlimaibu #mountibu #indonesia #kisiwa #h#halmahera #mlipuko #voa #VOASwahili