Azimio inaitaka serikali kuondoa kabisa Mswada wa Fedha

  • | Citizen TV
    4,262 views

    Muungano wa Azimio La Umoja umeipa serikali ya Kenya Kwanza makataa ya hadi saa sita usiku wa leo kutupilia mbali mswada wa fedha wa mwaka 2023 na kuchapisha mswada mpya la sivyo haitashiriki mazungumzo yoyote ya maridhiano. Wabunge wa Azimio wamekashifu vikali serikali kwa kupendekeza kuwatoza wakenya ushuru zaidi ilhali tayari wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha