Benki Kuu yasema Worldcoin haikuwa na leseni

  • | Citizen TV
    2,398 views

    Gavana wa Benki Kuu Kamau Thugge ameeleza bunge kuwa wamiliki wa kampuni ya sarafu za kidijitali Worldcoin hawakuwa na leseni kutoka CBK. Akihojiwa na kamati maalum ya bunge iliyobuniwa kuchunguza mchakato mzima wa Worldcoin Thugge aliongeza kuwa kima cha shilingi bilioni 1.2 zilizolipwa wakenya 350,000 baada ya kusalimisha taarifa za mboni zao hazikutambulika na cbk wakati biashara hiyo ilikuwa ilkiendelea. Huku hayo yakijiri, baadhi ya wakenya waliopokea malipo hayo sasa wanadai kuwa na matatizo ya macho wakitaka kujua deta yao inatumika vipi.