Changamoto za ukosefu wa hatimiliki za shule Busia

  • | Citizen TV
    417 views

    Uhaba wa ardhi na ukosefu wa hatimiliki katika baadhi ya shule na taasisi za umma katika kaunti ya Busia zimesalia changamoto kuu katika juhudi za kupanda miti shuleni. Wakizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa shule ya msingi ya Malaba kwa kuwa bora zaidi katika utunzi wa mazingira, afisa wa misitu kaunti ya Busia Vitalis Osodo pamoja na afisa msimamizi wa shirika la Linda Mazingira Patrick Ikwara wamewaomba wasimamizi wa shule kuhakikisha kuwa wanapata hatimiliki.