Familia ya Irene Gakwa, muuguzi aliyepotelea Marekani yataka majibu

  • | Citizen TV
    832 views

    Familia moja katika eneo la Rongai kaunti ya Kajiado inaomba serikali ya Marekani kuharakisha uchunguzi wa kutoweka kwa binti yao aliyekuwa akifanya kazi kama muuguzi katika jimbo la Gillete nchini humo. Familia ya Irene Gakwa inataka mwanamume anayedaiwa kuwa mpenziwe na aliyekutana na bintiye kwenye mitandao ya kijamii kujibu maswali aliko binti yao.