Familia zaidi ya 200 lazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko Bomet

  • | Citizen TV
    2,315 views

    Zaidi ya familia mia mbili maeneo bunge la Bomet mashariki na Bomet ya kati wamelazimika kuacha nyumba zao na kuishi katika shule moja kufuatia mafuriko yanayoshuhudiwa maeneo hayo. Wanakijiji hao wa rahia na chebirir wasema kuwa wamepoteza mazao yao baada ya kusombwa na maji. Mito iliyoko kwenye maeneo hayo imefurika huku daraja la itare kaptien limefurika maji. Wakazi hao wanaomba usaidizi wa bidhaa muhimu kama vile chakula, malazi, sabuni, maji safi na bidhaa zinginezo wakisema wanapitia changamoto si haba kambini.