Felix atoa wito kwa wahisani kumfadhili kujiunga na chuo kikuu cha Kabarak

  • | KBC Video
    16 views

    Huku shughuli ya wanafunzi ya kujiunga na chuo kikuu ikiendelea, Felix Kimanzi amejipata katika wakati mgumu kwani familia yake haiwezi kumlipia karo ya masomo yake ya chuo kikuu. Felix alikamilisha mtihani wake wa kitaifa wa masomo ya shule ya upili na kupata alama ya B wastani lakini hana uwezo wa kulipa karo inayohitajika ya shilingi 132,000 ya kujiunga na chuo kikuu cha Kabarak. Kimanzi alipokea barua ya kujiunga na chuo hicho ili kusomea kozi ya uanasheria tarehe 4 mwezi huu lakini bado yupo nyumbani. Sasa anatoa wito kwa wahisani kumsaidia ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasheria.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News