Fundi wa viatu mlemavu ateuliwa katika bunge la Siaya

  • | Citizen TV
    3,598 views

    Frederick Odhiambo, mkaazi wa Siaya na ambaye anaishi na ulemavu na pia ni fundi wa viatu ni mwakilishi wadi, baada ya chama cha ODM kumteua kuiwakilisha katika bunge la kaunti ya Siaya. Odhiambo ambaye aliwacha masomo akiwa katika shule ya msingi kwa kushindwa kugharamia masomo sasa atawakilisha maslahi ya walemavu katika bunge la Siaya.