Hatma ya hazina ya ustawishaji maeneobunge waibua wasiwasi

  • | Citizen TV
    1,081 views

    Hatma ya hazina ya ustawishaji maendeleo ya maeneobunge imezua jekejeke si tu miongoni mwa wabunge bali pia wakenya haswa kwa manufaa yake ya basari za masoko. Maeneo bunge nchini kwa muda yamejivunia miradi iliyojengwa na hazina hiyo ya CDF tangu mwaka wa 2013. Eneo bunge la Kibra kwa mfano limepiga hatua kubwa hasa katika sekta ya masomo, shule zaidi ya tano zikijengwa na mgao wa pesa za NG-CDF.