Jamii imetakiwa kuwasaidia wasichana wachanga wanaopata watoto

  • | Citizen TV
    261 views

    Jamii imehimizwa kutowatenga wasichana wanaopata watoto wakiwa na umri mdogo na badala yake kuwapa uwezo wa kukimu mahitaji ya familia zao. Haya yamesemwa kwenye kikao kilichoandaliwa katika eneo la Nyali kaunti ya Mombasa na shirika la Taji Langu kwa ushirikiano na Hospitali ya Wellcare kuwasherehekea kina mama waliopata watoto wakiwa wachanga. Shinikizo likitolewa kwa jamii kuwakumbatia wazazi hao ambao mara nyingi hujipata wakizidiwa na mzigo wa ulezi.