Jinsi pesa za Covid-19 zilivyotumika katika kaunti ya Nakuru

  • | K24 Video
    189 views

    Fedha za kudhibiti kuenea kwa virusi vya covid-19 zilizotengewa kaunti ya Nakuru zinazidi kuimarisha sekta ya afya miaka miwili baada ya janga. hospitali ya nakuru level 5 ilianzisha tenki za kuzalisha oksijeni ambazo ni kubwa zaidi katika maeneo ya kusini mwa jangwa la Afrika. Tenki hizo zina uwezo wa kuzalisha lita 2000 za oksijeni kwa dakika moja hatua ambayo imezidi kuokoa maisha wa maelfu ya wagonjwa katika maeneo ya bonde la ufa. japo miradi iliyoanzishwa inazidi kuwafaa wakazi wa Nakuru maswali kuhusiana na matumizi ya shilingi milioni 602 zilizotengwa na serikali kuu yameibuliwa na kufanyiwa ukaguzi na vitengo tofauti ikiwemo ofisi ya mkaguzi mkuu wa mahesabu wa serikali na kituo cha kuimarisha demokrasia na utawala, CEDGG.