Jopo linalowachunguza makamishna wa IEBC laanza vikao

  • | Citizen TV
    1,057 views

    Jopo la kumchunguza Kamishna wa IEBC aliyesimamishwa kazi Irene Masit limeanza kusikiliza malalamishi dhidi ya Kamishna huyo. Wakili wa Masit Donald Kipkorir alikuwa amepinga kuanza kwa kesi hiyo mbele ya jopo linaloongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Aggrey Muchelule. Wakili Donald Kipkorir alisema kesi hiyo inahusisha ushahidi mpya wa hatikiapo ambao haukutolewa katika kamati ya bunge kuhusu sheria, wakati malalamishi dhidi ya makamishna wanne wa IEBC yaliangaziwa. Jaji Muchelule hata hivyo alitupilia mbali upinzani wa Masit, kwa sasa Mlalamishi Dennis Nthumbi anaendelea kutoa malalamishi yake dhidi ya Masit.