Kaunti ya Kajiado yasitisha mikataba yote ya kaboni

  • | Citizen TV
    246 views

    Serikali ya kaunti ya Kajiado imepiga marufuku shuguli zozote zinazohusu hewa ya kaboni hadi pale kutakuwepo na mkataba mwafaka baina ya wakazi na kampuni zinazoendesha shuguli hiyo katika kaunti ya Kajiado. Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku anasema wakazi wengi wameingia kwenye mikataba ya kuruhusu shuguli za hewa ya kaboni kwenye mashamba yao bila ufahamu wa kutosha kuhusu shuguli hiyo. Akisem Kuna haja ya kuwepo kwa mazungumzo upya kabla ya shuguli hiyo kupewa idhini na serikali ya kaunti. Kauli yake imeungwa mkono na Waziri wa Utalii Penninah Malonza ambaye ameitaka wizara ya mazingira kutoa mwongozo dhabiti ambao utahakikisha wananchi wananufaika bila kuhadaiwa.