KBC na shirika la Bethel Network ilishuhudia kutolewa kwa sodo kwa wanafunzi wa Shule ya upili

  • | KBC Video
    12 views

    Swala la kukomesha kwa unyanyapaa unaohusishwa na maswala ya hedhi lilitawala mazungumzo wakati wa hafla moja iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji nchini-KBC huko Thika. Hafla hiyo iliyofadhiliwa na KBC na shirika la Bethel Network ilishuhudia kutolewa kwa sodo kwa wanafunzi wa Shule ya upili ya Joytown huko Thika katika Kaunti ya Kiambu huku kukiwa na wito wa kumuelimisha mtoto wa kiume kuhusu maswala ya hedhi ili kupunguza unyanyapaa na kuimarisha usafi wa hedhi miongoni mwa wanafunzi wa kike. Mwanahabari wetu Nancy Okware akiwa anasimulia zaidi kuhusu hafla hiyo iliyoambatana na nyimbo na densi huku wanafunzi wakidhihirisha talanta zao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News