Kifo cha mwanamke wa miaka thelathini kutoka Kibwezi kaunti ya Makueni

  • | K24 Video
    498 views

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanataka uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia kifo cha mwanamke wa miaka thelathini kutoka Kibwezi kaunti ya Makueni aliyepotea kwa njia tatanishi na mwili wake kupatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Mutomo kaunti ya Kitui. Mwili wa Nuru Akbar aliyepotea tarehe 29 machi mwaka huu ulipatikana katika mto athi katika eneo la Kiaoni kwenye mpaka wa kaunti za Makueni na Kitui ukiwa na majeraha. mshukiwa mkuu ambaye inadaiwa kuwa mumewe marehemu, Gideon Muthami ametiwa mbaroni na anazuiliwa katika kituo cha kibwezi