Kiongozi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji aonya kumshtaki Matiangi asipothibitisha madai yake

  • | K24 Video
    355 views

    Aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani daktari Fred Matiangi sasa yuko mashakani iwapo hatathibitisha madai kuwa maafisa wa polisi walifika katika boma lake la karen kwa nia ya kumkamata. Hii ni baada ya kiongozi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji kusema kuwa anapanga kumshtaki matiangi kwa kumhusisha rais William Ruto na matukio ya jana usiku. Haya yanajiri huku muungano wa kenya kwanza ukidai yaliyotokea jana ni sarakasi tupu kwani hakuna picha wala video zilizothibitisha maafisa wa polisi walifika nyumbani kwa Matiangi.