Koskei: Hakuna nyongeza ya mishahara na marupurupu

  • | KBC Video
    73 views

    Serikali inanuia kupunguza kiwango cha mishahara ya watumishi wa umma kutoka asilimia-46 hadi asilimia-35 ya bajeti kufikia mwaka-2028. Mkuu wa utumishi wa umma, Felix Koskei amesema serikali haitakubali shinikizo zozote za nyongeza ya mishahara na marupurupu katika sekta ya umma kutokana na mzigo mkubwa wa kiuchumi. Hayo yalijiri huku mwenyekiti wa tume ya kuratibu viwango vya mishahara ya watumishi wa umma-SRC, Lyn Mengich akionya kuwa taasisi yoyote ya serikali itakayoafikia mkataba wa maelewano na vyama vya wafanyikazi sharti iwe na pesa za kutekeleza mkataba huo la sivyo taasisi hiyo haitapokea mgao kutoka kwa serikali. Giverson Maina na taarifa kamili.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News