Kundi moja la vijana jijini Nairobi lachukua jukumu la kukuza miche ya matunda

  • | K24 Video
    80 views

    Kundi moja la vijana jijini Nairobi limechukua jukumu la kukuza miche ya matunda kupitia ukusanyaji wa mbegu ambazo kwa kawaida zingepotea katika masoko na shule. Miche wanayoikuza hupelekwa shuleni kupandwa. kujitolea huko sio tu ni kama njia ya kuhamasisha wanafunzi kuhusu umuhimu wa kupanda miti bali pia kuwapa motisha kwa kuwa wanafurahia matunda miti inapokomaa. Kulingana na mwenyekiti wa kundi hilo James Kamau, msimu huu wamegawa zaidi ya miche 10,000 kwa shule tofauti katika kaunti ya Nairobi pekee.