Madaktari wafanya upasuaji kwa kutumia teknolojia maalum Wajir

  • | Citizen TV
    264 views

    Wakaazi wa kaunti ya wajir na eneo la kaskazini mashariki kwa ujumla wana Kila sababu ya kutabasamu baada ya madaktari katika hospitali ya rufaa ya wajir kufanya upasuaji ya kwanza kutumia utaalamu wa kisasa kupitia njia ya matundu madogo ama Laparoscopy. Madaktari hao wameendesha upasuaji huo kupitia video iliyoko mbele yao. hii ni hospitali ya saba ya umma nchini na ya kwanza katika eneo la kaskazini mashariki kutoa huduma kama hii. Na kama anavyotuarifu mwanabari wetu abdikafar Hussein,ni afueni kwa wagonjwa ambao walikua walilazimika kusafiri hadi Nairobi ili kupokea upasuaji wa aina hiyo ambayo ilikua ikiwagharimu fedha nyingi.