Maina Njenga atoa msaada kwa waathiriwa Maai Mahiu

  • | Citizen TV
    1,742 views

    Kiongozi wa zamani wa Mungiki Maina Njenga pamoja na wazee wa baraza la wazee la jamii ya Agikuyu wametoa msaada wa vyakula na mavazi kwa waathiriwa wa mafuriko eneo la Maai Mahiu kaunti ya Nakuru. Viongozi hao wameunga mkono wito wa serikali wa kuwataka wale wanaoishi kwenye mabonde na mikondo ya maji kuhamia maeneo ya juu. akizungumza katika eneo hilo, Maina alieleza kuwa janga la mafuriko lililouwa watu zaidi ya 50 Maai Mahiu ndilo kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini. aidha ameitaka serikali kuharakisha shughuli za kuwatafutia makao waathiriwa.