Mamlaka ya mahakama Israeli yapunguzwa

  • | Citizen TV
    690 views

    Uamuzi wa serikali ya Israel wa kutekeleza sehemu ya kwanza ya sheria ya kupunguza nguvu za mahakama umesababisha ghasia katika mitaa ya taifa hilo na suitafahamu katika bunge la Knesset. Hata yanajiri huku Marekani ikitahadharisha utawala wa Israel dhidi ya kutekeleza mswada huo, ikitaja kupitishwa kwake kuwa bahati mbaya. Onyo hilo limetolewa huku maandamano ya raia yakishika kasi na kutishia nchi hiyo kuingia katika mgogoro wa kikatiba.