Mashirika ya misaada yatakiwa kuchukua hatua za haraka kushughulikia waathiriwa wa baa la njaa

  • | Citizen TV
    203 views

    Mashirika ya kutoa misaada kwa wa waathiriwa wa baa la njaa katika kaunti ya Garissa yamelaumiwa kwa kukosa kuwajibika kwa wakati unaofaa.Wakizumgumza baada ya kufungua kisima katika kijiji cha Aragaduud viungani mwa mji huo, mbunge wa Garissa mjini Mohammed Dekow alisema wakati umewadia kwa mashirika hayo kubadili mbinu na utaratibu wao wa kushughulikia majanga badala ya kuchukua muda mwingi kuidhinisha matumizi ya fedha za kutoa usaidizi. Aidha Aliitaka serikali kuu kugawa pesa za usawazishaji wa maeneo ili kusaidia katika mipango ya maendeleo. Kisima hicho kinatarajiwa kuwasaidia mamia ya wakaazi wa eneo hilo na viunga vyake kupata maji.