| MAZAO AFRIKA MASHARIKI | Wakulima waweka mikakati ya utoshelevu wa chakula

  • | Citizen TV
    1,604 views

    Eneo la Afrika Mashariki limekumbwa na changamoto za chakula kutokana na ukame uliotajwa kuwa mbaya zaidi katika miongo minne. Na huku mbingu zikiwa zimefunguka na mvua kunya, wakulima katika mataifa anzilishi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kenya, Uganda na Tanzania, yanaweka juhudi za kuhakikishia mataifa yana utoshelevu wa chakula. Kila taifa lina mbinu zake za uzalishaji ili kuboresha mazao na kutunza udongo na mazingira. Mashirima Kapombe alisafiri katika nchi jirani ya Uganda na kutuandalia makala haya ya kwanza, kwenye msururu wa makala ya mazao Afrika Mashariki.