Mkanganyiko kwa wazazi baada ya serikali kuahirisha kufunguliwa kwa shule

  • | Citizen TV
    4,071 views

    Wanafunzi na wazazi katika kaunti ya Kajiado wamejipata kwenye njia panda baada ya kufika shuleni na kupokea taarifa kuwa kufunguliwa Kwa shule Kwa muhula wa pili kumehairishwa hadi wiki ijayo. Wazazi waliokuwa tayari wamefika Kajiado Mjini wakipanga kuwapeleka wana wao kwenye shule zilizoko nje ya Kajiado walipatwa na mshangao Mkubwa baada ya kupata taarifa hizo wakiwa njiani kuelekea shule. wazazi hao wanasema Serikali ingepaswa Kutoa taarifa hiyo mapema. Wanafunzi wengi ambao walikuwa tayari wamewai shuleni katika shule ya msingi ya Kajiado township wamelazimika kurejea Nyumbani kuendelea na likizo Hadi wiki ijayo wakati shule zitafunguliwa baada ya ufunguzi kuahirishwa Kwa wiki Moja zaidi.