Mkimbizi mmoja kutoka DRC afariki kwenye kambi ya muda mjini Kitale

  • | Citizen TV
    285 views

    Idara ya afya katika kaunti ya Trans-Nzoia imedhibitisha mtu mmoja ameaga dunia katika kambi ya muda ya wakimbizi kutoka DRC mjini Kitale. Hiyo imefikisha kuwa wawili idadi ya watu waliofariki katika kambi hiyo katika muda wa chini ya wiki mbili, Haya yanajiri huku wakimbizi hao wakihitaji msaada wa dharura wa matibabu.