Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi afika mbele ya bunge kwa mara ya kwanza kujibu maswali

  • | K24 Video
    50 views

    Deni la taifa ,sasa limefikia trilioni 9.4. Haya ni kulingana na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi aliyefika mbele ya bunge kujibu maswali. Musalia amesema deni hilo kubwa limetikisa uchumi wa nchi kwani mgao mkubwa wa bajeti unagharamia madeni ya nje na ndani ya nchi. Hata hivyo, amesema serikali imeweka juhudi za kukwamua uchumi, akitaja mfano wa kununua mafuta ya petrol pasina kutumia fedha za kigeni. Waziri wa usalama Kindiki kithure na mwenzake wa ardhi Zachariah Njeru nao walikuwa mbele ya seneti kujibu maswali.