Moto watekeleza mali ya mamilioni ya pesa sokoni Wajir

  • | Citizen TV
    261 views

    wafanyibiashara katika soko kubwa zaidi kaunti ya wajir maarufu soko mjinga wanakadiria hasara ya mamilioni ya pesa baada ya moto mkubwa kuteketeza soko hilo. moto huo ambao chanzo chake bado hakijabainika, ulianza mwendo wa saa nne usiku na kuendelea kwa saa kadhaa huku wafanyibiashara wakishindwa kudhibiti kuzima moto huo. wakaazi wamenyoosha kidole cha lawama kwenye serikali ya kaunti kwa kutowajibika wakati moto huo ulianza kwani gari la wazimamoto halikuwa na maji wakati mkasa huo ulitokea. wafanyibiashara hao wametoa wito kwa serikali na mashirika yasiyo ya serikali kuwa saidia kuazisha biashara zao tena.