Mshukiwa afariki katika kituo cha polisi Taveta

  • | Citizen TV
    2,681 views

    Utata umeibuka kati ya maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Eldoro na wanakijiji wa eneo hilo katika eneobunge la Taveta kaunti ya Taita Taveta baada ya mshukiwa mmoja kufariki katika njia tatanishi. Roman Nyambu mwenye umri wa miaka 45 alikuwa amekamatwa kwa tuhuma za wizi siku ya Alhamisi tarehe 15 , kabla ya familia yake kujulishwa kuwa aliaga kwa kujitia kitanzi.