Mung'aro abadili msimamo wa kuondoa maiti Shakahola

  • | Citizen TV
    885 views

    Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro amebadili msimamo wake kuhusu kuondoa na kusafirisha miili ya waliouwawa katika msitu wa Shakahola hadi Nairobi. Hii ni baada ya kuzuru makafani ya hospitali ya malindi kukagua hali ya kontena zinamohifadhi miili hiyo.gavana huyo alikuwa ameapakuondoa miili hiyo akilalamika kuwa serikali ya kaunti inagharamia umeme kutokana na kwamba miili hiyo ilikuwa ikitoa harufu mbaya ambayo ilikuwa ikifika hata wadi alizozifanyia ukarabati na kuwekewa vifaa hivi majuzi.Mung’aro alisema kuwa baada ya kufanya ziara hiyo ya ukaguzi, imebainika kuwa kontena hizo hazitumii umeme kama inavyodaiwa awali.