Musa Hasahya Kasera: 'Nina wake 12, watoto 102 na wajukuu 568'

  • | BBC Swahili
    857 views
    Mwanakijiji kutoka Uganda, Musa Hasahya Kasera, anasema familia yake kubwa inajumuisha wake 12, watoto 102 na wajukuu 578. “Nimekuwa na matatizo mengi, kutafuta fedha za karo ya shule, kutoa chakula kwa kila mtu, kutafuta nguo na fedha za kusaidia endapo mtu anaumwa,” alisema mzee wa miaka 68 ambaye alipendekeza wake zake wachukue vidhibiti vya uzazi ili familia yao iache kukua. Kuoa wake wengi ni halali nchini Uganda, nchi yenye viwango vya juu zaidi vya kuzaliwa duniani, ambapo ni asilimia 50 tu ya wanawake wanapata udhibiti wa kisasa wa uzazi, kulingana na UN Women. "Alipoleta mwingine (mke), nakumbuka nilijisikia vibaya sana na hasira. Lakini baada ya muda nilizoea yote," alisema mke wa tatu wa Masa, Zabina Hasahya. #bbcswahili #uganda #familia