Mwalimu Peter Namasaka atuzwa kwa kuwatafutia wanafunzi ufadhili katika kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    233 views

    Wanafunzi pamoja na wazazi ambao walipata Ufadhili kupitia kwa Mwalimu mmoja huko Kajiado walijumuika Nyumbani kwake kumpa shukurani kutokana na juhudi zake za kuwatafutia ufadhili wa masomo. Wazazi pamoja na wanafunzi wamepongeza Juhudi za mwalimu huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akiwatafutia wanafunzi ambao hawana uwezo wa kulipa karo ufadhili ambapo zaidi ya wanafunzi 50 wamenufaika na mpango huo .