Naomi ni mchezaji wa kwanza mwenye asili ya Ethiopia kuingia timu ya wanawake ya taifa Marekani

  • | VOA Swahili
    2,082 views
    Naomi Girma akiongea na waandishi wa habari wakati wa siku ya waandishi ya Kombe la Wanawake la Dunia kwa niaba ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Marekani. “Nafikiri hili ndilo tunalotarajia. Unajua, kila mmoja atakuwa mpinzani shupavu katika hili Kombe la Dunia na katika kundi letu. Hivyo, sawa, nafikiri ni vile tulivyokuwa tumetarajia…” Timu ya Marekani ilishinda mechi yake ya kwanza katika Kombe la Dunia, magoli 3-0 dhidi ya Vietnam. Mechi inayofuata kwa Wamarekani ni dhidi ya Uholanzi --- timu ambayo Marekani iliishinda katika fainali ya Kombe la Dunia 2019 – huko Wellington Alhamisi. -AP #womensworldcup #2023FIFAWomensWorldCup #worldcup #uswnt #naomigirma #fifa #football - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.