Raila Odinga asema muungano wa Azimio umefikisha saini milioni 10

  • | K24 Video
    34 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga amesema muungano huo sasa umefikisha saini milioni 10 ambazo ni katika juhudi za kumbandua mamlakani Rais William Ruto na serikali yake ya Kenya Kwanza. Azimio itatoa mwelekeo wake katika siku zijazo lakini maandamano hayatakuwa katika mikakati ijayo ya kukabili Kenya Kwanza. Yamesemwa hayo leo katika hafla ya kutoa ripoti ya tathmini ya mwaka wa kwanza ya uongozi wa kenya kwanza. Azimio imempa Rais Ruto alama ya asilimia 30 ya utendakazi.