Rais Ruto aagiza wizara zote kuongoza katika upanzi wa miti kwa miezi 6 ijayo

  • | KBC Video
    77 views

    Rais William Ruto ameagiza wizara zote kuongoza katika shughuli ya upanzi wa miti katika kipindi cha miezi 6 ijayo kuanzia Jumatatu ili kufanikisha ajenda ya serikali ya kuafikia asilimia 30 ya utandu wa miti humu nchini kufikia mwaka wa 2032. Akiongea baada ya kuwaongoza wakenya katika shughuli ya kitaifa ya upanzi wa miti katika msitu wa Kiambicho, Kaunti ya Murang'a, Rais akizifariji familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na mafuriko, alisema kuwa njia pekee ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile mafuriko na ukame, ni kupanda miti akiwahimiza wakenya kuunga mkono mpango huo. Na kama anavyotuarifu Timothy Kipnusu, Rais Ruto wakati uo huo alisema serikali inaendelea kuhamisha watu walionyemelea maeneo yaliyo karibu na mito.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive