Rais Ruto atetea mpango wa ushuru wa nyumba za bei nafuu

  • | Citizen TV
    383 views

    Kwa mara nyingine tena Rais William Ruto ametetea mpango wa serikali wa kupendekeza ushuru wa asilima 3 wa hazina ya nyumba za bei nafuu akisema ni muhimu kuwasaidia Wakenya wa mapato ya chini kupata makao bora. Katika mahojiano ya moja kwa moja na wanahabari rais alisema mpango wa nyumba za bei nafuu unawiana na ule wa kuwapa vijana ajira kutokana na ujenzi wa nyumba hizo. Rais pia akizungumzia maswala kadhaa yakiwemo uchumi wa taifa pamoja na yanayojiri shakahola kama anavyotuarifu Chemutai Goin.