Ruto ahimiza bara Afrika kuchukua hatua mwafaka kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga

  • | KBC Video
    73 views

    Rais William Ruto ametoa wito kwa bara la Afrika kuchukua hatua muafaka ili kufanikiwa katika juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga. Kiongozi wa taifa ambaye alifungua rasmi mkutano wa tatu kuhusu jukumu la idara za mahakama katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga barani Afrika, alisisitiza haja ya kuwepo kwa haki katika upatikanaji wa fedha za kutosha za kusaidia bara hili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga. Majaji wakuu 30 na wakuu wa jumbe kutoka mataifa mbali mbali ya Afrika wanahudhuria mkutano huo wa siku tatu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #TheGreatKBC #climatechange