Sekta ya afya yapunguziwa fedha kwenye bajeti ya mwaka wa 2023/24

  • | K24 Video
    18 views

    Ndoto ya afya bora kwa wote imekuwa moja ya malengo kuu ya rais William Ruto, ila bajeti yake ya kwanza imepunguza mgao wa fedha kwa sekta ya afya kwa shilingi bilioni tano nukta sita, ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa 2022/23. Ndani ya bajeti hiyo kuna nyongeza ya kipengee cha mfumo wa dijitali utakaorahisisha utoaji huduma za afya hospitalini, pamoja na nyongeza ya bajeti kwa baadhi ya hospitali za rufaa.