Serikali yasimamisha uajiri wa wafanyakazi zaidi

  • | Citizen TV
    1,862 views

    Serikali imetangaza kuwa imepiga marufuku kuajiriwa kwa wafanyikazi wapya katika sekta ya umma bila ushauri kutoka kwa kamati ya taasisi za serikali. Waziri wa hazina kuu Profesa Njuguna Ndung'u akilalamikia gharama ya juu ya mishahara ya wafanyikazi wa umma ameitaka kamati hiyo kupiga msasa utendakazi wa wafanyikazi katika taasisi za serikali na kuhakikisha waliopo ni wale tu wanaohitajika.