Serikali yatoa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko Kisumu

  • | Citizen TV
    570 views

    Msemaji wa serikali Isaac Mwaura anatarajiwa katika eneo la Nduru kaunti ya Kisumu kutoa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko. Vijiji vitatu katika eneo hilo vimegubikwa na maji huku serikali ya kaunti ikisema kuwa watu mia sita wamekosa makao. Mafuriko katika kaunti ya Kisumu yalianza baada ya mto Nyando kuvunja kingo zake huku viwango vya maji vya Ziwa Viktoria vikiongezeka.