Shughuli za usafiri katika barabara kuu ya Mai Mahiu kuelekea Narok zakwama kufuatia mvua kubwa

  • | Citizen TV
    1,332 views

    Shughuli za usafiri katika barabara kuu ya Maai Mahiu kuelekea Narok zimekwama kufuatia mvua iliyonyesha wakati wa usiku. Mvua hiyo ikiharibu barabara na kuwatatiza wenye magari na kusababisha msongamano mkubwa. Picha za angani zinaonyesha athari ya mafuriko ambayo yalisomba nyumba za watu na kuharibu mashamba katika vijiji vya Kikuyan, Nairegi Enkare na Mosiro. Kufuatia hali hiyo watu 800 walioathirika sasa wametafuta makao ya muda katika shule ya msingi ya Oloosidan