Sulwe FM yadhimisha miaka 15 tangu kuasisiwa

  • | Citizen TV
    195 views

    Stesheni ya radio ya Sulwe FM inayomilikiwa na kamupuni ya Royal Media Services imeadhimisha miaka 15 tangu kuasisiwa. Idhaa ya Sulwe FM hupeperusha matangazo yake kwa lugha ya Kibukusu. Msimamizi Mkurugenzi wa Habari na Teknolojia katika kampuni ya Royal Media Services Fred Afune akiwashukuru wasikilizaji kutoka eneo la Magharibi kwa kufanya kituo cha Sulwe kutawala mawimbi ya utangazaji kwa miaka 15 na kutoa ahadi ya kuboresha vipindi vyake. Aidha Gavana wa Bungoma Ken Lusaka ametaja kituo cha redio cha Sulwe FM kama ambacho kimetoa mwelekeo kwa wenyeji wa jamii ya Mulembe kisiasa, kijamiii na kiuchumi na kwamba Sulwe ni raslimali kubwa kwa watu wa Magharibi ya Kenya.