Takriban marais 20 kuhudhuria hafla ya kumuapisha rais wa 5 wa Kenya

  • | Citizen TV
    2,355 views

    Marais wapatao 20 ni miongoni mwa wageni waalikwa wanaotarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa na kutawazwa kwa William Ruto kuwa rais wa tano wa Jamuhuri ya Kenya. Wanakamati wa kamati ya mpito wakiongozwa na katibu katika wizara ya usalama Karanja Kibicho, wamedokeza kuwa matayarisho ya siku hiyo ya kihistoria yanatarajiwa kukamilika kufikia kesho jioni.