Trump na Biden wanafursa katika sera ya bhangi uchaguzi mkuu

  • | VOA Swahili
    262 views
    Bhangi ni suala nadra la makubaliano katika Amerika iliyogawanyika kisiasa, huku ukusanyaji maoni ukionyesha kwamba asilimia 88 ya Wamarekani wanaunga mkono walau kwa kiasi fulani kuhalalisha bhangi. Lakini watetezi wa bhangi wanasema hakuna mgombea hata mmoja wa juu wa urais anatumia mitazamo inayobadilika. Takriban robo tatu ya Wamarekani wanaishi katika majimbo ambako bhangi ni halali kutumiwa kwa ajili ya matibabu. Nusu ya idadi ya watu wanaishi katika maeneo ambako bBhangi inaruhusiwa kwa starehe. Lakini Bhangi bado inaendelea kutizamwa kuwa si halali kwa mujibu wa sheria ya serikali kuu, ambako imewekwa pamoja na heroine na LSD kama dawa isiyo ya matumizi ya matibabu yanayokubalika kwa hivi sasa na kuna uwezekano mkubwa ikatumiwa vibaya. Idadi kubwa ya wapiga kura wa Marekani ambao wanadhani kwamba ni vyema mabadiliko yafanyike kwa bhangi ni fursa muafaka kwa wagombea urais Joe Biden na Donald Trump, hasa miongoni mwa wapiga kura vijana, kwa mujibu ….. . … Scotty Smart, ambaye ni mratibu wa jumuiya katika kundi la kiraia la New Georgia Project. Scotty Smart, New Georgia Project anaeleza: “Watu wengi hawaelewi sera. Watu wengi hawafahamu jinsi sera zinavyoathiri maisha ya kila siku. Nadhani banghi ni suala ambalo linachochea na kuwasisimua vijana wadogo kulipa mtizamo.” Caroline Phillips, National Cannabis Festival amesema: “Kwa wote hao, jambo moja ambalo wanafana ni kwamba rekodi yao juu ya bhangi imekuwa haiendani na inaongezeka. Tumesikia ahadi kutoka kwa tawala zote mbili, hakuna hata moja ambaye amejitokeza wazi wazi.” #bhangi #marekani #siasa #wamarekani #wagombea #urais #uchaguzi #voa #voaswahili #dunianileo #donaldtrump #joebiden