Viongozi wa Kenya Kwanza waunga mkono mazungumzo baina ya Azimio na serikali

  • | Citizen TV
    454 views

    Spika wa bunge la Taifa Moses Wetangula aliongoza viongozi wa Magharibi ya Kenya kuunga mkono mazungumzo ya maridhiano kati ya muungano tawala wa Kenya Kwanza na ule wa Azimio la Umoja. Akizungumza kwenye hafla ya kuchangisha fedha za kujenga bweni katika shule ya upili ya wasichana ya St. Anne Musoli, eneo bunge la Ikolomani, kaunti ya kakamega, Wetangula amesema kwamba taifa linahitaji amani ili kunawiri kiuchumi.