Viongozi wa makanisa kaunti ya Samburu wataka serikali kukaza kamba katika ukaguzi wa makanisa

  • | Citizen TV
    488 views

    Viongozi wa makanisa kaunti ya Samburu wamejitosa kwenye mdahalo wa mahubiri ya itikadi potofu ikitaka serikali kukaza kamba katika ukaguzi wa makanisa nchini. Askofu wa kanisa la kiangilikana ACK Jimbo la Maralal David Lebarlaiya na mwenzake wa kanisa Katoliki Eronmas Njoya wametaka udhibiti mkali wa makanisa yanayochipuza. Haya yameibuka kufuatia kuibuka kwa utata wa mahubiri tata ya Paul Mackenzie katika kaunti ya Kilifi.