Viongozi wahimizwa kufanya kazi pamoja Kakamega

  • | Citizen TV
    621 views

    Baadhi ya viongozi katika kaunti ya kakamega sasa wanawataka viongozi waliochaguliwa nchini kusahau tofauti zao za mirengo ya kisiasa na badala yake kuwafanyia wananchi wote kazi. Wakizungumza wakiwa na kundi la wanajamii la 42 Changers kule shikomari kaunti ndogo ya Navakholo Kakamega walitoa hamasisho kuhusu umuhimu wa demokrasia nchini kauli mbiu ikiwa kuwahusisha wanajamii kuchunguza utendakazi wa serikali ya kaunti. viongozi hao wamesisitiza kuwepo kwa amani na ushirikiano baina yao ili kutimiza miradi ya maendeleo. Aidha wameitaka serikali ya kaunti kushirikiana na mashirika ya kijamii yenye maono ya kuboresha maisha ya wanajamii .