Visa vya dhuluma kwa watoto vimeratibiwa kuongezeka kaunti ya Garissa

  • | Citizen TV
    236 views

    Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya idadi ya watu, imebainika kuwa kaunti ya Garissa imenakili ongezeko la mimba za mapema, dhulma za kijinsia na maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi. Kulingana na utafiti ya mwaka wa 2014, asilimia kumi nukta moja ya wale walio na kati ya miaka kumi na kumi na tisa katika kaunti hiyo tayari wamepata watoto.Hali hii imechangiwa pakubwa na mila potovu na ukeketaji ambapo msichana wa umri mdogo hupitia tohara na kuozwa kwa wazeeUtumizi wa mihadharati miongoni mwa vijana katika eneo hilo pia yamechangia kuwepo na visa vya ubakaji, dhulma ya kijinsia na kuongezeka kwa visa vipya vya ukimwi.